Klabu ya Guangzhou            Evergrande imemsajili kiungo wa            Tottenham Paulinho kwa pauni milioni 9.8 huku Mbarazil huyo            akianguka mkataba wa miaka minne.
        Paulinho anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye            jina kubwa kuondoka Tottenham katika kipindi hiki ambacho            kocha Mauricio Pochettino anataka            kukifumua kikosi chake.
        Kiungo huyo sasa anakwenda kuungana na            kocha wa zamani wa Brazil Luiz            Felipe Scolari ambaye ndie kocha mkuu wa klabu hiyo Guangzhou Evergrande.
        Paulinho, 26 ameshindwa kudumisha kiwango            chake alichokuwa nacho wakati anajiunga na Tottenham kwa pauni            milioni 17 miaka miwili iliyopita.
        Guangzhou Evergrande                ya china imemsajili Paulinho kwa pauni  milioni 9.8 
        Paulinho (kulia)                enzi zake akiwa na Tottenham
           Luiz Felipe Scolari                kocha wa Guangzhou                Evergrande 
          
Comments
Post a Comment