PATRICK VIEIRA APONDA WANAOBEZA BEI YA RAHEEM STERLING …kauli yake yapingana na Rio Ferdind


PATRICK VIEIRA APONDA WANAOBEZA BEI YA RAHEEM STERLING …kauli yake yapingana na Rio Ferdind
PATRICK VIEIRA amemfagilia Raheem Sterling na kuwaponda wanaosema ni ujinga kwa Manchester City kumnunua winga huyo kwa zaidi ya pauni milioni 40.
Mabosi wa Etihad Stadium wanatajwa kutenga pauni milioni 50 kwa nyota huyo wa Liverpool baada ya ofa zao za pauni milioni 30 na 40 kupigwa chini.
Hiyo itamfanya Sterling awe mchezaji ghali zaidi Uingereza kuliko yeyote yule huku baadhi ya watu wakisema hana thamani hiyo.
Lakini Viera ambaye kwa sasa ni anangoza academy ya City, amesema winga huyo wa kimataifa wa England ana vigezo vyote vya kununuliwa kwa bei mbaya.
Raheem              Sterling
KIPAJI KILICHO TUKUKA: Vieira anaamini Sterling ana thamani ya kila pesa itakayotolewa 
""Nadhani kama ukiwauliza watu 10 nini wanachofikiri juu yake, tisa watamkubali."
Patrick Vieira
Alisema: "Nadhani kama ukiwauliza watu 10 nini wanachofikiri juu yake, tisa watamkubali.
"Binafsi ningekuwa sehemu ya watu hao tisa kwasababu Rahim amethibitisha ubora wake.
"Kama akiwa sokoni, sio City peke yake itakayohangaika kumsajili".
Chelsea, Paris Saint-Germain na Real Madrid zote zilionyesha nia ya kusaka saini ya Sterling.
Patrick                Vieira
DOLE TUPU: Vieira anaamini Sterling utakuwa ni usajili mzuri kwa City
Hivi karibuni mchezaji wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand aliponda bei zinazotolewa kwa wachezaji wa Kiingereza akiwemo Raheem Sterling ambaye alisema wazi kuwa hana thamani ya kununuliwa kwa pauni milioni 4o.


Comments