Ngoma akisaini
Mshambuliaji nyota kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma amesaini miaka miwili kuichezea Yanga.
Ngoma pamoja na kiungo Joseph Zuttah 'Tetteh' naye amesaini miaka miwili kuichezea Yanga.
Tetteh akisaini Wote wawili jana walifanyiwa vipimo vya afya na kufuzu na leo wakafanya mazoezi na kikosi cha Yanga kabla ya kusaini mkataba leo. |
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Isaac Chanji kwa kushirikiana na Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha ndiyo walishirikiana kukamilisha zoezi hilo.
Comments
Post a Comment