Nathaniel Clyne amepigwa picha akitokea            hospitali ya Liverpool mara baada ya kufanya vipimo vya afya            Jumatatu hii katika hatua za kuelekea kukamilisha usajili wake            kutoka Southampton.
        Beki huyo wa kulia anakwenda Liverpool kwa            pauni milioni 10.5 huku baadae zikitakiwa kuongeza pauni            milioni 2 kadri maendeleo yake yatakavyokuwa Anfield.
        Nathaniel Clyne aliyekuwa pia akiwaniwa na            Manchester United, anakuwa mchezaji wa sita kutua Liverpool            kiangazi hiki.
        Nathaniel                akitokea hospital ya Liverpool akiwa amemaliza kufanya                vipimo vya afya
        Clyne  kutangazwa                rasmi Liverpool muda wowote kuanzia sasa
        
Comments
Post a Comment