NATHANIEL CLYNE KUKAMILISHA USAJILI WAKE LIVERPOOL WIKI IJAYO



NATHANIEL CLYNE KUKAMILISHA USAJILI WAKE LIVERPOOL WIKI IJAYO
NATHANIEL CLYNE atakamilisha usajili wake Liverpool wiki ijayo baada ya Southampton kukubali ofa ya pauni milioni 12.5.
Beki huyo wa kulia wa England atajadiliana kuhusu maslahi binafsi na Liverpool na hatimaye kufanya vipimo vya afya mara baada ya kumaliza mapumziko yake wiki ijayo.
Clyne, 24,  anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano  Liverpool na kuungana na nyota wengine watano Roberto Firmino, James Milner, Danny Ings, Adam Bogdan na Joe Gomez  waliosajiliwa Anfield kiangazi hiki.
WIKI IJAYO: Nathaniel Clyne atajiunga na Liverpool wiki ijayo
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajia Clyne ataimarisha beki ya kulia baada ya  Glen Johnson kuondoka.


Comments