NA HAYA NDIO MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU FIRMINO WA LIVERPOOL


NA HAYA NDIO MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU FIRMINO WA LIVERPOOL

fil

Roberto Firmino amejiunga na Liverpool kwa ada ya paun 29m.Mashabiki bado wanahamu ya kujua zaidi kuhusu huyu mchezaji kutokana na jinsi anavyoendelea kuisaidia nchi yake kwenye michuano ya Copa America. Hivi hapa ni vitu muhimu ambavyo vitakusaidia kumjua zaidi Firmino.

ASILI

Firmino alizaliwa Maceio huko Brazil. Alianza maisha ya soka na timu ya vijana ya Clube de Regatas Brazil kabla ya kujiunga na Figueirense.

ALIVYOIBUKA

Firmino alianza kucheza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka17 Oktoba 24, 2009 alipoingia kama mchezaji wa akiba kipindi cha pili. Alipata namba ya kudumu mwezi januari na kufunga goli lake la kwanza 2010. Alifanikiwa kuirudisha katika ligi kuu klabu yake ya Figueirense baada ya kukosa kwa kipindi cha misimu miwili.

BARANI ULAYA

Desemba 2010 alisajiliwa moja kwa moja kujiunga na Hoffenheim ya Bundesliga ya Ujerumani. Goli lake la kwanza ilikuwa 2011 na la ushindi dhidi ya Eintrancht Frankfurt. Alitangazwa mchezaji bora anayechipukia mwaka 2011 baada ya kufunga mara 16 katika michezo 33.

USHAWISHI 

Firmino ana rekodi ya pasi 21 za magoli (assists) ndani ya misimu miwili iliyopita zaidi yam brazil yeyote anayecheza katika ligi kubwa zote tano duniani. Barani Uropa pekee kafunga magoli 47 ndani ya michezo 151.

TIMU YA TAIFA

Mechi yake ya kwanza timu ya taifa ilikua dhidi ya Uturuki novemba 12 mwaka jana. Alifunga goli lake la kwanza katika timu ya taifa siku sita baadae dhidi ya Austria, na hadi sasa amefunga mara nne katika michezo 9.

FITNESS

Kutokana na majeraha yote yanayomsibu mshambuliaji Daniel Sturridge wa Liverpool, hali ni tofauti kwa Firmino ambaye kacheza mara 33 kati ya mechi 34 za Hoffenheim msimu uliopita. Ni kicheko kwa Brendan Rodgers.

MATARAJIO

Usajili wa Roberto Firmino wa paun 29m unamfanya kuwa wa pili nyuma ya Andy Carrol aliyesajiliwa kwa paun 35m. matarajio ni makubwa na hakuna shaka uwepo wa Phillipe Coutinho utamfanya Firmino afanye anachokifanya sasa na timu yake ya taifa.

 



Comments