Manchester United imerudisha majeshi katika kusaka saini ya Bastian Schweinsteiger na ili kuongeza ushawishi, itamhakikishia mamba ya kudumu iwapo atakubali kuhamia Old Trafford.
Kiungo huyo wa Ujerumani bado hajaamua hatma yake kwa Bayern Munich - yuko njia panda, abaki au aondoke na kuweka rehani uhakika wa kucheza kila mechi.
Lakini kocha wa United Louis van Gaal anajiandaa kumpa uhakika wa namba ya kudumu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la Times.
United inaandaa ofa ya pauni milioni 17.8 ili kumpata Schweinsteiger mshindi wa kombe la dunia.
Comments
Post a Comment