MANCHESTER UNITED YAPELEKA RASMI OFA YA KUMTAKA SERGIO RAMOS WA REAL MADRID ...yaweka mezani mzigo wa pauni mil. 35
Manchester United imepeleka rasmi ofa yao kwa Real Madrid ikitaka kumsajili sentahafu Sergio Ramos.
Inaaminika kuwa ofa ya Manchester United ni ya pauni milioni 35 ambayo imekuja muda mfupi baada ya Ramos kuwaambia maofisa wa Real Madrid kuwa anataka kuondoka.
Mtendaji mkuu wa Real Madrid Jose Angel Sanchez alikutana na wakala wa Ramos, Rene Ramos ambaye pia ni kaka wa beki huyo lakini badala ya kufikia maafikiano, ndio kwanza Ramos akaomba maongezi na United yaanze.
Inaaminika ofa hiyo haitegemei mgongo wa David de Gea anayetegemewa kwenda Real Madrid lakini inaaminika United itatumia maombi yao hayo ya kumsajili Ramos kufikia makubaliano ya kumuuza kipa wao kwa miamba hiyo ya Hispania.
Manchester United imepeleka maombi ya kumsajili Ramos kwa pauni milioni 35
Ramos (kulia) Jumatano iliyopita aliwaambia maofisa wa Real Madrid kuwa anataka kuondoka
David de Gea huenda akatua Real Mdrid
Comments
Post a Comment