MANCHESTER UNITED YAPANIA KUJIBU MAPIGO YA LIVERPOOL KWA KUMSAJILI CARLOS BACCA ...ni baada ya kupigwa bao kwa Roberto Firmino


MANCHESTER UNITED YAPANIA KUJIBU MAPIGO YA LIVERPOOL KWA KUMSAJILI CARLOS BACCA ...ni baada ya kupigwa bao kwa Roberto Firmino
Bacca is a              target for several Premier League clubs
KAZI IPO: United inamtaka Bacca ambaye anawaniwa na Liverpool

Manchester United imedhamiria 'kumteka nyara' mshambuliaji wa Sevilla Carlos Bacca anayewaniwa na Liverpool.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia amelivutia jicho la kocha wa United Louis van Gaal baada ya kuwa na msimu mzuri kwa timu yake na nchi yake.
Liverpool tayari imeshasajili wachezaji watano kiangazi hiki: Adam Bodgan, Danny Ings, James Milner, Joe Gomez na Roberto Firmino na sasa Bacca anakuwa chaguo linalofuata kwa kocha Brenden Rodgers.
Lakini kwa mujibu wa gazeti la Telegraph Uingereza, United inaongoza mbio za kumsajili Bacca.
Roberto Firmino alikuwa ananukia kujiunga na Manchester United lakini dakika za mwisho Liverpool wakaingia na kufanikiwa kumsajili kiungo huyo wa Brazil kwa pauni milioni 29.



Comments