MANCHESTER UNITED YALAMBA DUME KWA KUMSAJILI DAYOT UPAMECANO



MANCHESTER UNITED YALAMBA DUME KWA KUMSAJILI DAYOT UPAMECANO

Sentahafu kinda Dayot Upamecano inayeaminika kuwa tayari amesaini kujiunga na Manchester United, anatajwa kama beki bora anayeinukia duniani akiwa na uwezo wa hali ya juu wa kumiliki mpira pamoja na umadhubuti wa kucheza mipira ya juu.
Manchester United imeripotiwa kukubali kukamilisha dili la uhamisho wa staa wa Valenciennes ya Ufaransa, Dayot Upamecano na kuzipiga kumbo Manchester City na Arsenal.
Kwa mujibu wa mtandao wa Tuttomercatoweb, United imekubali dili linaloaminika kuwa karibu pauni 700,000 kuweza kupata saini ya beki huyo wa kati, raia wa Ufaransa.
Habari zinasema kuwa Upamecano mwenye umri wa miaka 16 hatapelekwa moja kwa moja kikosi cha kwanza, lakini anaonekana kuwa msaada mkubwa siku za mbele.
Arsenal ilikuwa ikimfukuzia kwa karibu beki huyo mwenye uwezo wa kupanda mbele kusaidia mashambulizi, lakini Van Gaal amecheza vizuri karata zake.


Comments