MANCHESTER UNITED YAIKOMALIA REAL MADRID, YASEMA BILA PAUNI MIL 35 DE GEA HAN'GOKI OLD TRAFFORD ...ni hasira za kunyimwa Sergio Ramos
Manchester United imetanua mbavu zake kwa Real Madrid na kuwaambia bila pauni milioni 35, hawampati De Gea ng'oo.
United iko tayari kumtumia De Gea kwa msimu            mzima ujao na baadae kuodoka bure kuliko kumtoa kipa huyo  kwa            bei ya kutupa.
        Hatua hiyo inaonekana ni kama ya kulipa kwa            Real Madrid ambayo imekataa ofa ya pauni milioni 35 ya            Manchester United kumtaka beki Sergio Ramos.
        De Gea, 24 aliyejiunga na United mwaka 2011            kwa pauni milioni 17.8 amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba            wake Old Trafford na ataondoka bure kiangazi kijacho.
        Ada ya pauni milioni 35 kwa De Gea itakuwa            ni rekodi mpya kwa magolikipa duniani, ikivunja rekodi ya Gianluigi Buffon aliyenunuliwa na Juventus            kwa  pauni milioni 32 kutoka Parma mwaka 2001.
        Manchester United                imeikomalia Real Madrid juu ya usajili wa De Gea 
        De Gea anatakiwa na                Madrid huku United nao wakimtaka Sergio Ramos 
        United wanataka £35m                kwa  De Gea -ambayo itamfanya awe kipa ghali zaidi mbele                ya Gianluigi Buffon wa Juventus
          
Comments
Post a Comment