MANCHESTER UNITED YAIAMBIA REAL MADRID IAMUE KUSUKA AU KUNYOA KUHUSU DE GEA NA RAMOS



MANCHESTER UNITED YAIAMBIA REAL MADRID IAMUE KUSUKA AU KUNYOA KUHUSU DE GEA NA RAMOS

Mabosi wa Manchester United wameisisitizia Real Madrid kuwa  De Gea hatauzwa labda tu kama watapewa Sergio Ramos.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez sasa anasema Ramos thamani yake ni  pauni million 40 na anataka wapewe De Gea pamoja na pauni milioni 20 kutoka United. 
Mwanzoni ilisemwa Real wanamtaka De Gea na pauni milioni 40 huku Perez akimthaminisha Ramos kwa pauni milioni 145.
Lakini mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward anajua ni jinsi gani Perez amepania kumpata De Gea kiangazi hiki na hivyo amepanga kuwakomalia miamba hiyo ya Hispania.
Daily Star la Uingereza linaandika kuwa United ipo tayari kumuona De Gea anamalizia mkataba wake wa miezi 12 iliyobakia iwapo Real Madrid watakataa kufuata matakwa yao.
Licha ya kuwa De Gea, 24 atakuwa huru kiangazi kijacho lakini United inaamini Real Madrid watakuwa na kipa huyo kwa miaka 10 ijayo huku thamani yake ikizidi kuongezeka. 
Kimahesabu, United inaona kumnunua Ramos kwa bei mbaya ni hasara kwasababu beki huyo mwenye umri wa miaka 29 atakuwa hana thamani pindi mkataba wake utakapomalizika Old Trafford.
United ina jeuri ya pesa na hivyo haiofii kuendelea kukaa na De Gea kwa mwaka mmoja zaidi na kumwacha aondoke bure na kupoteza pauni milioni 20 ambazo ingezipata kwa kumuuza. 
KUSUKA AU KUNYOA: United intake bishara ya kubailishana kwa Sergio Ramos na David De Gea, suala pesa juu yake HAKUNA!
Ramos anabanwa na mkataba lakini inadaiwa ameshawaambia  Real kuwa anataka kutimka.
Barcelona ilionyesha nia ya kumtaka Ramos lakini Perez akakataa kumuuza sentahafu huyo kwa wapinzani wao wakubwa.
Hiyo inazidi kuwapa jeuri United ambayo sasa imewaachia Real Madrid waamue kusuka au kunyoa.



Comments