MANCHESTER UNITED KUMPELEKA DI MARIA PSG ILI WAPEWE CAVANI



MANCHESTER UNITED KUMPELEKA DI MARIA PSG ILI WAPEWE CAVANI

MANCHESTER UNITED inataka kufanya biashara kubwa ya kubadilisha wachezaji na Paris St Germain  - Angel Di Maria aende kwa mabingwa wa Ufaransa na Edinson Cavani atue Old Trafford.

Winga wa Argentina Di Maria ambaye aliigharimu Manchester United pauni milioni 59.7 na kuwa rekodi mpya ya usajili England, amekuwa akizitoa udenda klabu kubwa barani Ulaya licha ya kuwa na wakati mgumu Old Trafford msimu uliomalizika.

Mabingwa wa Hispania na Ulaya Barcelona na mabingwa Ujerumani Bayern Munich wote wameonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid.

Hata hivyo United haina mpango wa kuuza silaha kwa wapinzani wao wakubwa wa Ulaya hususan Barcelona na Bayern.

Lakini klabu hiyo ya Old Trafford haioni tatizo kumpeleka PSG hasa kwa staili hii ya kubadilishana na Cavani mshambuliaji hatari wa kimataifa wa Uruguay anayetajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50.
KUBADILISHANA: Cavani kupishana na Di Maria 
Kocha wa United Louis van Gaal amekuwa akihaha kupata mshambuliaji mpya lakini amejikuta akikwama katika kila chaguo lake - Mario Mandzukic amekwanda Juventus huku Tottenaham wakiweka wazi kwamba Harry Kane hauzwi, wakati kocha huyo Mdachi akiona thamanii ya pauni milioni 32 kwa Christian Benteke ni bei kichaa.

Hiyo inamuacha Cavani, 28 kama mshambuliaji pekee wa kiwango cha kidunia anayeweza kufiti Old Trafford hususan kwa kubadilishana na Di Maria aliyeshindwa kuendana na mfumo wa timu.




Comments