LIVERPOOL YATHIBISHA KUMSAJILI ROBERTO FIRMINO …yampa mkataba wa miaka mitano, mshahara pauni 100,000 kwa wiki



LIVERPOOL YATHIBISHA KUMSAJILI ROBERTO FIRMINO …yampa mkataba wa miaka mitano, mshahara pauni 100,000 kwa wiki
Liverpool imethibitisha kumsajali kiungo mshambuliaji Roberto Firmino kwa ada ya pauni milioni 29 akitokea Hoffenheim  ya Ujerumani.

Klabu hiyo imesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 23 amekubali mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki.

Kilichobakia sasa ni kukamilishwa kwa hati za kufanyia kazi pamoja na vipimo vya afya kabla ya mchezaji huyo kutangazwa rasmi.
Attacking                    midfielder Roberto Firmino has completed his transfer                    to Liverpool for £29m
Kiungo mshambuliaji Roberto Firmino amekamilisha usajili wa pauni milioni 29 kwenda  Liverpool 
Firmino took                    part in Brazil training in Santiago and looked relaxed                    ahead of the official announcement
Firmino akiwa mazoezini na  Brazil huko  Santiago Chile 
The                    23-year-old hinted at a move away from German side                    Hoffenheim and Liverpool have sealed the deal
Firmino, 23 (kulia) aanaondoka Hoffenheim  ya German na kujiunga na Liverpool

WACHEZAJI WA BEI MBAYA LIVERPOOL

1) Andy Carroll - £35m - January 2011
2) Roberto Firmino - £29m - June 2015
3) Adam Lallana - £25m - July 2014
4) Luis Suarez - £22.8m - January 2011
5) Fernando Torres - £20.2m - July 2007
Manchester United ambayo msimu uliopita ilipwaya sana kwenye eneo la kiungo, ilikuwa ikimfuatilia kwa karibu Firmino baada ya kuvutiwa na kiwango chake kwenye Bundesliga msimu uliomalizika.


Wiki kadhaa, nyuma tetesi zilisema Firmino anatarajiwa kwenda Old Trafford kufanya vipimo vya afya mara tu Copa America itakapomalizika,  lakini Liverpool wamekuwa  wababe zaidi.

Liverpool watalipa pauni milioni 22 mwanzoni na kiasi kilichobakia kitalipwa baadae.





Comments