LIVERPOOL imeipiga bao la kisigino Manchester United baada ya kufikia maafikino ya kumsaji kiungo 'mtamu' wa Brazil Roberto Firmino kwa ada ya pauni milioni 29.
Dili hilo litakamilika Jumatano ambapo kiungo huyo wa Hoffenheim ya Ujerumani, atakuwa mchezaji wa pili wa bei mbaya kusajiliwa na Liverpool.
Andy Carroll aliyesajiliwa kwa pauni milioni 35 miaka kadhaa iliyopita kabla ya kupigwa bei baadae, ndiye anayeendelea kushikilia rekodi ya usajili wao wa bei mbaya Liverpool.
Mtendaji mkuu wa Liverpool Ian Ayre alikuwa Chile Jumanne kwaajili ya kujaribu kukamilisha usajili wa Firmino anayeitumikia Brazil kwenye michuano ya Copa America inayoendelea huko Chile.
Comments
Post a Comment