LIVERPOOL imeingia sokoni kusaka straika            mpya na rada zao sasa zimenasa kwa Mario Gomez wa Fiorentina            ambaye kwa mujibu wa mtandao wa Tuttomercatoweb anataka            kuondoka Serie A baada ya kuona makali yake yanapungua.
        Straika huyo wa kimataifa wa Ujerumani,            amefanikiwa kufunga mabao 10 tu msimu uliomalizika, lakini            anabaki kuwa staa tishio kwenye 18 za adui – sifa aliyokuwa            nayo tangu anaibuka hadi sasa.
        Gomez mwenye umri wa miaka 29, hadi sasa            amepiga mabao ya kuvutia 166 katika ligi ndani ya mechi 308            alizocheza kwa kipindi chake chote.
        
Comments
Post a Comment