LIVERPOOL WASITEGEMEE MAKUBWA SANA KWA ROBERTO FIRMINO



LIVERPOOL WASITEGEMEE MAKUBWA SANA KWA ROBERTO FIRMINO
Roberto Firmino had a night to forget as Brazil crashed              out at the Copa America on Saturday night

Liverpool wanategemea mengi makubwa kutoka kwa kiungo mshambuliaji wa Kibrazil aliyenunuliwa kwa pauni milioni 29, Roberto Firmino, lakini kiwango chake dhidi ya Paraguay kinatia mashaka.
Kwenye mchezo huo wa robo fainali ya Copa Amarica, Firmino alishindwa kung'ara kabisa huku 'pea' yake na Philippe Coutinho ambaye atakuwa nae Liverpool ikishindwa kutoa matunda.
Firmino alichezeshwa kama mshambuliaji namba tisa ambapo kwa muda wote wa mchezo alifanikiwa kufanya shambulio moja tu la maana.
Liverpool ina utajiri wa viungo  kama ilivyo Brazil na hivyo kitu pekee kitakachombeba Firmino ni uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi - anaweza akacheza kama winga wa kushoto na kulia au mshambuliaji wa kati.
Hata hivyo ni katika nafasi hizo za zaida ndizo zilizoonyesha ubutu wa kiwango chake kilichozoeleka kwenye nafasi yake ya kiungo mshambuliaji.
Firmino, Robinho, Willian, na Coutinho wote wanacheza soka ya aina moja - akili nyingi, uwezo wa kukokota mipira, chenga na watu wasiohofia kuwafuata mabeki - lakini hakuna hata mmoja wao anayeweza kujipambanua uwanjani kama mtu mwenye uwezo wa kuibeba timu. Na hilo ndilo lililo igharimu Brazil, baada ya kumkosa Neymar timu ikapotea.
Firmino alikuwa sehemu ya safu ya ushambuliaji ya Brazil iliyomudu kufunga magoli matano katika mechi 4 huku wenyeji Chile wakifunga magoli 11.
Baadhi ya wachambuzi wa soka wa michuano ya Copa America wamedai Liverpool isitegemee makubwa sana kutoka kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23.
Hata hivyo kiungo wa zamani wa Brazil Ronaldinho anaamini pacha ya Firmino na Coutinho itazaa matunda Liverpool akiwa na imani na nafasi wanazozitengeneza na magoli ambayo wamekuwa wakifunga.




Comments