Liverpool inajipanga kusajili mweingine kiangazi hiki baada ya kupeleka maombi ya kutaka kumsajili mshambuliaji tishio wa Aston Villa, Christian Benteke.
Tayari Liverpool imeshawanasa wakali watano kiangazi hiki Firmino, James Milner, Danny Ings, Adam Bogdan na Joe Gomez.
Liverpool pia inakaribia kumsajili beki wa Southampton Nathaniel Clyne kwa pauni milioni 12.5, hivyo Benteke anaweza kuwa mchezaji wa saba kutua Anfield.
Baada ya kuwasajili wapishi wengi wa magoli, sasa Rodgers anaona ni wasaa wa kusajili 'muuaji'.
Katika hilo, Benteke, 24, anakuwa chaguo kuu ingawa hakuna uhakika sana kama Liverpool watamudu kufikia kipengele cha manunuzi cha pauni milioni 32 iwapo Villa watadengua kufanya biashara.
Comments
Post a Comment