LIVERPOOL MAMBO SAFI ...OFA YAO YA KUMSAJILI NATHANIEL CLYNE YAKUBALIWA NA SOUTHAMPTON ....anakuwa mchezaji wa sita kutua Anfield
SOUTHAMPTON            imekubali ofa ya pauni milioni 12.5 ya Liverpool kwaajili ya            usajili wa full beki Nathaniel            Clyne ambaye atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Brenden            Rodegrs kiangazi hiki.
        Liverpool ilibisha hodi Southampton muda mfupi baada              ya kumnasa kiungo mshambuliaji wa Kibrazil Firmino            kwa ada ya pauni milioni 29 akitokea Hoffenheim            ya Ujerumani
        Clyne, 24, ataungana na              Firmino, James Milner, Danny Ings, Adam Bogdan na Joe Gomez              ambao nao wanatua  Anfield kiangazi hiki.
        
Comments
Post a Comment