Morgan Schneiderlin ameonekana akiwasili Southampton tayari kwa mazoezini ya kujiandaa na msimu mpya licha ya kiungo huyo Ufaransa kuwa mbioni kutua Manchester United kwa pauni milioni 25.
Mkali huyo mwenye umri wa miaka 25 amepigwa picha Jumatatu akiwasili mazoezini akiwa sambamba na mchezaji mpya aliyesajiliwa kiangazi hiki Maarten Stekelenburg.
Kikosi cha Southamton kimeanza mazoezi mapema Jumatatu hii tayari kwa kujiandaa na michuano ya Europa League mwishoni mwa mwezi Julai.
Schneiderlin anatarajiwa kutangazwa rasmi kujiunga na Manchester United wiki hii.
Morgan Schneiderlin (kushoto) akiwasili kwenye uwanja wa wazoezi wa Southampton akiwa sambamba na mchezaji mpya Maarten Stekelenburg
Kiungo wa Southampton Schneiderlin anatarajiwa kujiunga na Manchester United
Schneiderlin alinyimwa kuondoka St Mary msimu uliopita lakini safari hii klabu yake imekubali kumuuza
Comments
Post a Comment