LICHA YA KUMSAJILI CEDRIC SOARES SOUTHAMPTON YATAKA PAUNI MIL 15 KWA NATHANIEL CLYNE …Liverpool ni juu yao kusuka au kunyoa



LICHA YA KUMSAJILI CEDRIC SOARES SOUTHAMPTON YATAKA PAUNI MIL 15 KWA NATHANIEL CLYNE …Liverpool ni juu yao kusuka au kunyoa

LIVERPOOL imeripotiwa kujiandaa kukamilisha uhamisho wa  wa beki Nathaniel Clyne baada ya klabu yake ya Southampton kumsainisha Cedric Soares lakini imeambiwa ni lazima iweke mezani pauni milioni 15, kinyume na hapo hakuna biashara.
Southapmton imesisitiza kuwa licha ya kumsajili Cedric Soares, haitakubali kumwachia Nathaniel Clyne kwa pesa inayopungua pauni milioni 15.
Kwa mujibu wa gazeti la Express, Southampton haionekani tena kuwa kikwazo cha kuondoka beki huyo wa kiamataifa wa England baada ya kusajili mbadala wake, lakini si kwa bei ya kutupwa.
Gazeti hilo limeandika kuwa kilichobaki sasa ni makubaliano ya ada ya uhamisho baada ya Southampton kuitolea nje ofa ya pauni milioni 10 iliyotolewa awali na Liverpool.
Baada ya Glen Johnson kuondoka, Liverpool imekuwa katika mawindo ya beki mpya wa kulia na klabu hiyo inaamini Clyne mwenye miaka 24 ni mtu bora wa kucheza nafasi hiyo.



Comments