Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie anaweza akaondoka Old Trafford kiangazi hiki.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal aliyejiunga na Manchester United kiangazi cha mwaka 2012, alishindwa kuwa namba ya kudumu chini ya Loius van Gaal msimu uliopita na akatumia muda mwingi kama chaguo la pili nyuma ya Wayne Rooney.
Mapema wiki hii, Van Persie, 31 amegusia kuwa anaweza akaondoka Old Trafford kama hata hakikishiwa namba ya kudumu.
Kwa mujibu wa mtaalam wa soka wa Holland, Marcel van der Kraan, kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo akaondoka Manchester United kiangazi hiki.
"Uwezekano wa yeye kuondoka ni mkubwa, ndio ni mkubwa sana," Van der Kraan ameliambia gazeti la Daily Star.
Robin van Persie ameeleza utashi wa kupata uhakika wa namba ya kudumu wakati akitathmini hatma yake Manchester United
Van Persie kwa sasa yupo likizo huko Miami akiwa na mkewe Bouchra pamoja na watoto wao
Van Persie na mkewe Bouchra wakifurahia mapumziko
Van Gaal alishasema hivi karibuni kuwa Manchester haina mpango wa kumuuza Van Persie na kwamba yupo kwenye mipango yake ya msimu ujao.
Hata hivyo kocha huyo alimtaka Van Perisie akaze buti mazoezi na kudhihirisha kuwa yupo fiti, vinginevyo atajikuta akikaa benchi.
Comments
Post a Comment