Na Bertha Lumala, Mbeya
'Hivi karibuni Jerry Muro alitozwa faini ya Sh. milioni tano kutokana na kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)."
Wakati Yanga leo wamesisitiza kuwa walimsajili kiungo Gofrey Mwashibhuya akiwa mchezaji huru, uongozi wa Kimondo FC umemtuhumu Muro kuudhalilisha kupitia vyombo vya habari anapozungumza juu ya sakata hilo.
Akiwa zirani mkoani Mtwara leo, mkurugenzi na mlezi wa Kimondo FC, Erick Ambakisye, ameuambia mtandao huu kuwa Mwashibhuya ni mchezaji halali wa timu yake na ana mkataba, hivyo Yanga wafuate utaratibu wa kumsajili na wasitake suala hilo lifikishwe mbele ya vyombo vya sheria vya TFF.
"TFF iliagiza kila timu inayoshiriki Ligi Kuu na zile zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kuhakikisha zinawapa wachezaji wao mikataba na ndicho sisi tulichokifanya kwa wachezaji wetu akiwamo huyo mtoto Geofrey Mwashibhuya. Timu yoyote inayomtaka mchezaji wetu, lazima ifuate taratibu za usajili," amesema Ambakisye.
Mkurugenzi huyo amedai kuwa maneno yaliyosemwa Muro alipozungumza na moja ya vituio vya redio vya Dar es Salaam ni maneno ya kumdhalilisha akiwa kiongozi wa wananchi (diwani) ambao wanamwamini.
Comments
Post a Comment