JUAN SEBASTIAN VERON: NYOTA ILIYOSHINDWA KUNG’AA OLD TRAFFORD


JUAN SEBASTIAN VERON: NYOTA ILIYOSHINDWA KUNG'AA OLD TRAFFORD

verob

Na Simon Chimbo;

Usajili wa kiungo Juan Sebastian Veron bila shaka unasemwa kua mbovu zaidi kuwahi kutokea katika historia ya klabu ya Manchester United na ligi kuu ya nchini Uingereza. Kijana huyo raia wa Argentina alizaliwa tarehe 9 march 1975 huko La Plata, Argentina. Pamoja na kupitia timu nyingi kubwa kama Boca Juniors, Sampdoria, Parma na Lazio, Veron alijikuta akitua mikononi mwa kocha Sir Alex Ferguson wa Manchester United akitokea Lazio mwaka 2001 kwa ada ya uhamisho wa paun 28m za Uingereza, pesa nyingi zaidi kwa kipindi hicho huku akiingia katika rekodi ya usajili wa pesa nyingi zaidi ulimwenguni. Bila shaka Veron alikua na kiwango cha dunia hata kupelekea magwiji hao wa kandanda wa Uingereza watoe kiasi hicho.

Historia yake fupi

Juan Sebastian Veron ni mtoto wa kwanza wa mchezaji wa zamani na mshambuliaji wa Estudiantes na timu ya taifa ya Argentina, Juan Ramon Veron. Baba yake Juan, mzee Juan Ramon Veron aliwahi kuifunga goli timu ya Manchester United mwaka 1968 Old Trafford akiichezea Estudiantes ya Argentina katika michuano ya Intercontinental Cup.

Juan Sebastian Veron alizaliwa siku baba yake, Ramon akicheza katika mechi ya watani wa jadi kati ya Estudiantes na Gimnasia y Esgrima. Akiwa kijana Veron alikua na ndoto za kuichezea Sheffield United ya Uingereza timu aliyokua akiichezea mjomba wake wakati huo, Pedro Verde. Alipoanza kucheza soka ya kulipwa, baba yake alianza kuishawishi klabu aliyowahi kuichezea yeye ya Panathinaikos ili imsajili, lakini baada ya kufanya majaribio alijikuta akishindwa kufanya vizuri na kusajiliwa na timu pia aliyowahi ichezea baba yake ya Estudiantes de La Plata mnamo mwaka 1993 huku akiisaidia kurudi katika ligi kuu ya Argentina mwaka 1995. Mwaka 1996 alisajiliwa Boca Juniors aliyokua anaichezea mchezaji mahili zaidi Ulimwenguni Diego Maradona na kucheza mechi 17 huku akiifungia magoli matatu. Aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina mwaka huo huo na kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Poland. Muda mchache baadae alisajiliwa na kocha Sven-Goran Eriksson na kujiunga nae Sampdoria ya Uitaliano.

Nchini italia;

Baada ya kuichezea timu ya taifa ya Argentina katika fainali za kombe la dunia mwaka 1998, Veron alijiunga na Parma kwa ada ya uhamisho wa paundi 15m, msimu uliofuata Parma wakashinda Coppa Italia na kombe na Ulaya(uefa cup). Eriksson akamsajili kwa mara nyingine tena mara hii akiwa anaifundisha Lazio kwa ada ya paundi 18.1m huku akilipwa mshahara wa wa paundi 48,000 kwa wiki. Aliichezea Lazio kwa mara ya kwanza dhidi ya Manchester United na kupata ushindi wa 1-0 katika mechi ya European Super Cup, mjini Monaco. Mwaka 2000 Juan Sebastian Veron alikua ni roho ya Lazio huku wakifanikiwa kutwaa ubingwa wa Italia maarufu kama 'scudetto', Coppa Italia na Italian Super Cup.

Lakini mnamo februari, 2000 alijikuta katika uchunguzi wa Polisi kwa kilichodaiwa kufoji Paspoti ya Italia kukwepa tozo ya wachezaji ambao sio wazawa wa umoja wa Ulaya. Lakini alifanikiwa kukwepa adhabu baada ya kugundulika kua passport yake ni halali kwani alipewa na maafisa wa Italia wenyewe.

Msimu wa 2000-2001 mnamo Julai 12' alijiunga na klabu ya Manchester United kwa uhamisho wa kihistoria katika soka la uingereza wa ada ya paundi 28.1m usajili ghali zaidi wakati huo. Alikaliliwa akisema haofii kucheza ligi kuu ya Uingereza.

Maisha yake Uingereza, Manchester United; 

Kama ni usajili ulioteka hisia za mashabiki wengi duniani kote hususan wa mashetani wekundu ni usajili wa kiungo huyo muagentina Juan Sebastian Veron. Akiwa old Trafford, tofauti na matarajio ya wengi alijikuta hadi leo anatajwa kama usajili mbovu zaidi katika historia ya klabu. Alihangaika kuendana na kasi ya mpira wa kiingereza 'pace' kitaalamu. Baadae aliondoka kwenda Chelsea ambako hata hivyo alishindwa kuwaVeron wa zamani.



Comments