Mlinzi na nahodha wa            zamani wa Simba, Joseph Owino amejiunga na timu ya Sofapaka            inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.
        Mlinzi huyo wa zamani wa            SC Villa na URA FC aliichezea Simba kwa vipindi viwili tofauti            kabla ya kuamua kuondoka baada ya msimu uliopita kuisha            kutokana na kusugua benchi.
        Owino ambaye pia aliwahi            kuichezea Azam fFC anaungana na Mganda mwenzake, Herman Wasswa            ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo            Ijumaa iliyopita.
        Akiwa Sofapaka, beki huyo            mganda atakuwa chini ya kocha kutoka nchini kwao, Sam Timbe.
        
Comments
Post a Comment