Mipango ya Arsenal imekwenda kombo baada ya mshambuliaji chaguo lao la kwanza kwenye usajili Jackson Martinez kuamua kujiunga na Atletico Madrid.
Wakala wa mchezaji huyo Luiz Henrique Pompeo amethibisha kuwa Martinez amechagua Atletico Madrid badala ya Arsenal na AC Milan.
Pompeo amesema: "Kila kitu kimekamilika. Atletico ni klabu kubwa ambayo imefanya mengi makubwa kwenye La Liga na Ligi za Ulaya.
"Jackson anakwenda pale kupigania mataji na kuonyesha ubora wake na kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi. Ilikuwa ni njozi yake na amevutiwa sana. Kwa hakika ni mwenye furaha."
Comments
Post a Comment