ILKAY GUNDOGAN AYEYUKA OLD TRAFFORD …aamua kubaki Borussia Dortmund



ILKAY GUNDOGAN AYEYUKA OLD TRAFFORD …aamua kubaki Borussia Dortmund

Ilkay Gundogan ameyeyuka Old Trafford baada ya kuamua kubakia  Borussia Dortmund, hiyo ni kwa mujibu wa  Bild am Sonntag gazeti maarufu la nchini Ujerumani.
Manchester United ilikuwa ikihusishwa na uhamisho wa pauni milioni 20 kwa Gundogan na akatangaza mapema kiangazi hiki kuwa hana mpango wa kusaini mkataba mpya Dortmund.
Lakini kwa mshangao wa wengi kiungo huyo amepiga 'U-turn' na kukubali kusaini mkataba mpya utakaomweka Dortmund hadi mwaka 2017.


Comments