Kama kama kweli Barcelona wanahitaji kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Angel Di Maria basi italazimika kulipa pauni milioni 85.5.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina hana furaha Old Trafford baada ya kuanza vibaya kwa msimu wake wa kwanza Manchester United.
Imebainika kuwa wakati Real Madrid inamuuza Di Maria kwa Manchester United, iliweka kipengele kinachomzuia mchezaji huyo kurejeshwa Hispania kwa ada iliyo chini ya pauni milioni 85.5.
Kwahiyo ili Barcelona imnase mkali huyo ni lazima ivunje benki na kulipa pauni milioni 85.5.
Bayern Munich pia ilikuwa inamtaka Di Maria lakini sasa imehamishia nguvu zake kwa Douglas Costa wa Shakhtar Donetsk ambaye anawaniwa pia na Chelsea.
Barcelona watalazimika kulipa £85million kama kweli wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Angel di Maria
Di Maria amekiri hakuwa na msimu mzuri Manchester United
Comments
Post a Comment