HUENDA ILKAY GUNDOGAN AKATUA MANCHESTER UNITED WIKI IJAYO … Borussia Dortmund yafungua njia




HUENDA ILKAY GUNDOGAN AKATUA MANCHESTER UNITED WIKI IJAYO … Borussia Dortmund yafungua njia Manchester United inaweza ikaangaza usajili wa Ilkay Gundogan wiki ijayo.
Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la The Daily Express ambalo limemnukuu mtendaji wa Borussia Dortmund Michael Zorc akisema kuna wachezaji  wataondoka klabuni kwao siku chache zijazo.
Ripoti zinasema inaminika Gundogan ni miongoni mwa walengwa wa Zorc na hiyo ni baada ya United kupeleka ofa ya pauni milioni 21 kwa miamba hiyo ya Bundasliga. 
Ilkay Gundogan Man Utd transfer              news
OLD TRAFFORD: Gundogan huenda akatua United wiki ijayo
"kutakuwa na matukio ya wachezaji kuondoka wiki ijayo"
Michel Zorc
Inasemekana United wako kwenye maongezi na Gundoga na dili linaweza likakamilika mapema
Zorc alisema: "Kuna wachezaji wetu tutakaowapoteza kiangazi hiki.
"Kutakuwa na matukio yatakayoibuka kuanzia wiki ijayo"


Comments