HIVI NDIVYO LIVERPOOL WANAWEZA KUCHEZA MFUMO WA 3-4-3 MSIMU UJAO



HIVI NDIVYO LIVERPOOL WANAWEZA KUCHEZA MFUMO WA 3-4-3 MSIMU UJAO
Liverpool's Brendan Rodgers
Graphic kutoka kwa mchambuzi mmoja wa soka imesambaa kwenye mitandao ikionesha mfumo mpya wa Liverpool wanaoweza kutumia msimu wa 2015-16 ambao ni 3-4-3.
Kikosi hicho cha Liverpool kimewashangaza wengi kutokana na Nathaniel Clyne kuanzishwa upande wa kushoto.
Clyne, ambaye anatarajia kukamilisha usajili wa kujiunga na Liverpool kutokea Southampton kwa dau la paundi milioni 12.5 ni beki wa kulia kiasilia, lakini kaanza sehemu tofauti.
Mchambuzi huyo amejaribu kadri awezavyo kuwaingiza kwenye kikosi cha kwanza wachezaji wapya wa Liverpool na amependekeza kwamba,  Danny Ings anaweza kucheza mbele na  Daniel Sturridge, huku Roberto Firmino, Jordan Henderson na  Philippe Coutinho wakicheza safu ya kiungo.
Wakati huo huo,  James Milner, aliyejiunga na Liverpool kutoka Man City akipangwa kucheza kwa mapana kutoka winga ya kulia, huku kushoto akipangwa   Alberto Moreno.
 Adam Lallana hajapata nafasi ya kuanaza.
Tazama Graphic hapa chini ikionesha kikosi cha kwanza cha Liverpool;


Comments