Mshambuliaji Harry Kane ameitolea mbavuni Manchester United kwa kusema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuondoka Tottenham.
Baada ya kuwa na msimu mzuri, Harry Kane sasa amekuwa nguzo ya kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya miaka 21.
Umahiri wake wa kuzifumania nyavu ukaipelekea Manchester United imfanye moja ya malengo yao makubwa ya usajili wa kiangazi hiki na walikuwa tayari kuweka mezani pauni milioni 45.
Kane anasema Tottenham ni klabu kubwa na yuko na furaha kuendelea kuitumikia na kwamba suala la uhamisho kwa sasa halipo kwenye akili yake.
Harry Kane amesema hana mango wa kuondoka Tottenham
Kane (kushoto, akiwa na England Under 21) amekuwa akihusihwa na usajili wa kwenda Manchester United
Hivi karibuni Kane (katikati) alisaini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kuitumikia Tottenham
Comments
Post a Comment