Napoli imedhamiria kubaki na mshambuliaji            wao Gonzalo Higuain huku ikisema            hakuna klabu inayoweza kumng'oa bila pauni milioni 67 ambacho            ndicho kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake.
        Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina            ambaye kwasasa yupo Chile akiitumikia nchi yake kwenye            michuano ya Copa America, amekuwa akiwaniwa na Liverpool, Arsenal, Manchester City pamoja            na AC Milan.  
        Msemaji wa Napoli Nicolas Lombardo amesema hakuna nafasi ya Higuain kuondoka labda timu zifikie            kipengele hicho cha pauni milioni 67.
        "Napoli tumedhamiria kuweka wazi hili kwa            kutoa mwongozo rasmi kwamba Higuan ana kipengele cha manunuzi            cha pauni milioni 67.
        "Hakuna ofa itakayopokelewa chini ya            kiwango hicho, wote wanaomtaka mchezaji huyo ni lazima wafikie            thamani yake," anaeleza Lombardo            katika maongezi yake na Radio            Kiss Kiss ya Italia.
        Napoli hawana mpango                wa kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Argentina Gonzalo                Higuain mwenye umri wa miaka 27
        Higuain anakipengele                kinachomrushu kuondoka Napoli kwa pauni million 67
        
Comments
Post a Comment