Baada ya kufungashiwa virago katika michuano ya Copa America, mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani jana amemtembelea baba yake mzazi aliyefungwa gerezani.
Baba wa straika huyo wa PSG alitiwa mbaroni Jumatano ya wiki hii na kuswekwa gerezani kwa kosa la kumgonga muendesha pikipiki na alikuwa anaendesha gari akiwa amelewa pombe kinyume na sheria.
Mtu aliyegongwa alifariki baadaye na hii inamaanisha baba yake Cavani anakabiliwa na kosa la mauaji na kwasasa amefungwa katika gereza la mji wa Cañitas.
Cavani alienda kumtembele baba yake jana na aliweka wazi kwamba amefanya hivyo kwa lengo la kukagua hali ya Gereza kimazingira.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ni kwamba Cavani anafikiria kununua nyumba karibu na gereza hilo ili awe anamtembelea baba yake kila wiki.
Comments
Post a Comment