EDINSON CAVANI ‘AIPELEKA’ CHILE NUSU FAINALI YA COPA AMERICA …YAICHAPA URUGUAY 1-0, MAURICIO ISLA AIBUKA SHUJAA
Mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Copa America, ukashuhudia dakika 80 za mwanzo wenyeji Chile wakiibana Uruguay lakini wakakosa kabisa mbinu za kutupia mipira wavuni.
Wakati hatua ya matuta ikianza kunukia kwenye jiji la Santiango, Chile wakafanikiwa kuweka hai ndoto zao za kutwaa taji kubwa baada ya miaka mingi.
Mshambuliaji tegemeo wa Uruguay Edinson Cavani akafanya makosa mawili ya kijinga yaliyosababisha alambwe kadi mbili za njano zilizozaa kadi nyekundu dakika ya 63 na kuwapa ahueni kubwa wenyeji.
Uruguay walicheza zaidi mchezo wa kujihami huku wakiweka ukuta mgumu uliowatesa vijana Jose Sampoli lakini dakika 81 Mauricio Isla aliyewahi kuichezea QPR ya England kwa mkopo akaifungia Chile bao pekee.
Wakati mpira ukielekea ukingoni, Uruguay wakalambwa kadi nyingine nyekundu baada ya Jorge Fucile kutolewa kwa kumchezea rafu ya hatari Alexis Sanchez.
Chile wanatinga nusu fainali ambapo sasa watachuana na mshindi wa mchezo wa Bolivia na Peru utakochezwa Ijumaa.
Wenyeji wanapewa nafasi kubwa ya kutinga fainali na kukabialiana kati ya Argentina, Colombia, Brazil au Paraguay.
Mauricio Isla (katikati) akishangilia na wachezaji wa akiba wa Chile baada ya kuifunga bao pekee
Isla akifunga goli dakika ya 81
Edinson Cavani akilambwa kadi nyekundu
Cavani akionyesha kukerwa na maamuzi
Comments
Post a Comment