DI MARIA AKIRI MAMBO MAGUMU MANCHETER UNITED ...SAFARI YA BARCELONA NAYO YAYEYUKA



DI MARIA AKIRI MAMBO MAGUMU MANCHETER UNITED ...SAFARI YA BARCELONA NAYO YAYEYUKA

Winga wa Manchester United Angel Di Maria amekiri kuwa mambo yalimwendea kombo Old Trafford msimu uliomalizika.
Inadaiwa mchezaji huyo ghali zaidi kupata kutokea katika Ligi Kuu ya England, anaweza akatimka Manchester United baada ya kuwa na msimu mbaya.
Hata hivyo safari ya nyota huyo kwenda Barcelona kama ilivyoripotiwa hapo awali, haipo.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique alikuwa amejazwa matumaini ya kumnasa winga huyo baada ya wakala wake kumpigia chapuo ahamie Camp Nou.
Gazeti la Mundo Deportivo la Hispania limesema safari ya Di Maria kwenda Barcelona haiwezekani kwa kuwa Real Madrid wameweka kipengele kinachomzuia mchezaji wao huyo wa zamani asiuzwe kwa mahasimu wao wa La Liga.
HAENDI BARLCELONA: Di Maria hatajiunga na Barcelona 
Akizungumzia msimu wake uliopita, Di Maria alisema msimu ulikuwa mbaya kwake.
Di Maria aliliambia gazeti la Ole: "Ulikuwa mgumu kwangu? Ndio, kwangu na kwa familia yangu.
"Kwasababu sio kila kitu kilikwenda vizuri kama nilivyotaka, kwasababu sikucheza mechi nyingi.
"Kwasababu nilikwenda pale nikiwa na matarajio makubwa lakini nikaishia kusota benchi. Ni ngumu kukueleza nilivyojisikia.
"Nilianza vizuri kwa magoli pamoja na kusadia wafungaji wengine. Nikawa na wasaa mzuri kabla mambo hayajabadilika.
Ni ngumu kidogo kukueleza kwanini sikuchezeshwa."


Comments