COPA AMERICA: BRAZIL OUT, YATOLEWA NA PARAGUAY KWA MATUTA



COPA AMERICA: BRAZIL OUT, YATOLEWA NA PARAGUAY KWA MATUTA

Paraguay ikiwa imepewa nafasi finyu ya kufika nusu fainali ya Copa America, imefanya kisichotarajiwa baada ya kuitupa nje Brazil.

Katika mchezo huo wa robo fainali timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1 pale dakika 90 za kawaida zilipotimu na hivyo njia ya mikwaju ya penalti ikachukua nafasi yake.

Paraguay wakatupia wavuni michomo minne huku wakipoteza moja wakati Brazil walikosa penalti mbili na kupata tatu na hivyo kutolewa kwa jumla ya penalti 3-4.

Brazil ilikuwa ya kwanza kutangulia kwa bao la dakika ya 15 lililofungwa na mshambuliaji wao mzoefu Robinho.

Dakika ya 72, Paraguay wakapata penalti iliyopigwa vizuri na Derlis Gonzalez na kuzaa bao la kuzawazisha.

Paraguay sasa itakutana na Argentina katika mchezo wa fainali utakaopigwa Jumanne wakati nusu fainaili nyingi itaikutanisha Chile na Peru siku ya Jumatatu.


Comments