CHILE YATANGULIA FAINALI, YAISUBIRI ARGENTINA AU PARAGUAY ...tazama picha kibao namna walivyoichinja Peru
Nchi mbili pinzani zilizowahi kupigana vita vya Pacific karne ya 19, Chile na Peru zilikuwa na vita nyingine katika nusu fainali ya Copa America ambapo wenyeji wamesonga mbele kwa ushindi wa bao 2-1.
Hata hivyo mchezo huu unaacha mjadala mkubwa baada ya Chile kuonyesha soka bovu kabisa tangu michuano hii ianze lakini kwa kile kilichoonekana kama mbeleko ya refarii, timu hiyo ikatinga hatua ya fainali na sasa inasubiri mshindi kati ya Argentina na Paraguay.
Kitendo cha mwamuzi Jose Argote kumlamba kadi nyekundu Carlos Zambarano nacho kitachochea utambi katika mjadala mkubwa mingoni mwa mashabiki wa soka wa Peru.
Jose Argote alimpa kadi ya njano Zanbarano kunako dakika ya 7, kabla ya kumtoa nje dakika ya 20, hatua iliyochangia Chile kupata bao la kwanza kupitia Eduardo Vargas katika dakika ya 42.
Ingawa huwezi kumlamu Jose Argote kwa kumtoa Zambarano baada kumkanyaga mgongoni Charles Aranguiz, mwamuzi alikuwa na matukio mengi yaliyozua malalamiko kwa wachezaji wa Peru.
Zambarano aliokoa mpira wa juu kwa guu lake la kulia lakini mwisho wa siku mguu ule ukaishia kutua mgogoni mwa Aranguiz aliyedondoka huku akijishika mgongoni, mwamuzi hakuwa na kingine cha kufanya zaidi ya kutoa kadi nyekundu.
Peru wakasawazisha dakika ya 60 baada ya Gary Medel kujifunga katika juhudi zake za kuokoa.
Furaha ya Peru ikadumu kwa dakika nne tu kabla ya Eduardo Vargas mshambuliaji wa zamani wa QPR hajafunga tena katika dakika ya 64.
Mshambuliaji wa Peru Paolo Guerrero alisema: "Sitaki tena kuzungumzia kuhusu waamuzi, siku zote wameonyesha wako upande wa wenyeji."
Peru sasa watacheza katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu siku ya Ijumaa kati ya Argentina au Paraguay.
Eduardo Vargas amefunga mara mbili dhidi ya Peru na kuisadia Chile kutinga fainali ya Copa America
Eduardo Vargas akipiga shuti kufunga bao la pili kwenya Uwanja wa Taifa jijini Santiago
Kipa wa Peru Pedro Gallese akiruka bila mafanikio huku mpira ukitinga wavuni
Mguu wa Carlos Zambrano ukienda mgongoni mwa Charles Aranguiz
Carlos Zambrano anakula red card dakika ya 20
Wachezaji wa Chile wakishangilia baada ya mpira kumalizika
Wachezaji wa Chile wakiomba dua muda mfupi kabla mchezo hajaanza
Comments
Post a Comment