Chelsea imeanzisha mazungumzo na Stoke City juu kumpata kipa Asmir Begovic.
Masaa machache baada ya safari ya Petr Cech kwenda Arsenal kuthibitshwa, Chelsea imeanza kusaka mrithi wake ambapo Jose Mourinho anamuona mlinda mlango huyo wa Bosnia kama mtu sahihi.
Daily Mail la Uingereza linafichua kuwa Chelsea imepeleka ofa ya pauni milioni 6 kwaajili ya Asmir Begovic.
Hata hivyo inaaminika Stoke itakataa ofa huyo kutokana na ukweli kuwa inahitaji pauni milioni 10 ili kumwachia kipa huyo.
Mabingwa wa Premier League Chelsea wameanzisha maongezi na Stoke juu ya kipa Asmir Begovic
Jose Mourinho anamchukulia Begovic kama mtu sahihi wa kuziba nafasi ya Cech aliyetimkia Arsenal
Comments
Post a Comment