Chelsea itamtoa kiungo wake Oscar pamoja            na pesa kama sehemu ya dili la kumpata kiungo wa kimataifa wa            Ufarasansa na Juventus, Paul Pogba.
        Inaeleweka kuwa            kocha wa Juventus Massimiliano            Allegri ni shabiki mkubwa wa Oscar mwenye umri wa miaka 23            huku Chelsea ikiwa tayari kumwacha aondoke  Stamford Bridge.
        Oscar alifunga magoli 6 katika mechi 28 za            ligi alizocheza msimu uliopita alishuhudia nafasi yake ya            kucheza ikipunguzwa taratibu na sasa huenda akaondoka London.
        Chelsea inatarajiwa kupigana vikumbo na  Manchester City, Real Madrid, Barcelona na            Paris St-Germain kwa Pobga mwenye thamani ya pauni milioni 70.
        Kwa mujibu wa            gazeti la Mirror la Uingereza, ni kwamba Mourinho            atamtoa Oscar pamoja na pauni milioni 30 ili kunasa saini ya            Pobga.
        
Comments
Post a Comment