CARLOS TEVEZ: UGUMU WA MAISHA UTOTONI NA SIRI YA KOVU LAKE



CARLOS TEVEZ: UGUMU WA MAISHA UTOTONI NA SIRI YA KOVU LAKE

tevez

Simon Chimbo;

Watu wengi walipata kuyaona maandishi yaliyopo mbele ya T-shirt ya ndani ya mshambuliaji Carlos Tevez ambayo huonesha pale anaposhangilia goli, Fuerte Apache.

Fuerte Apache ni mtaa uliopo huko Buenos Aires Argentina. Hapa ni makao makuu ya uhalifu. Sio sehemu nzuri kuishi, pombe, madawa na uporaji wote hapa ndio ulipozaliwa, hapafai. Fuerte Apache ndio mtaa aliozaliwa mshambuliaji mwenye nguvu Carlos Tevez. Ni sehemu wanaishi watu masikini sana nchini Argentina.

"Ilikua ni kipindi kigumu sana kuishi Fuerte Apache, usiku unapoingia, giza kali, huwezi kutazama hata dirishani, ilikua inaogopesha sana. Huwezi kutembea hata mtaani, ni hatari" anasema Carlos Tevez

Kitu kilichobakia kumbukumbu kwake ni kovu lake la shingoni, uso na hadi kifuani. Ilikua ni ajali akiwa na miezi kumi tu tangu azaliwe aliungua na maji ya moto yaliyokua yakichemka jikoni.

Ilikua ni ajali mbaya kwa Tevez ambaye aliugulia kwa kipindi cha miezi miwili.  Tevez hata alipoanza kucheza soka aliamua kutunza kovu lake kama nembo ya uhalisia wa maisha yake na alikotoka.

Akicheza katika klabu yake ya kwanza kabisa kama mchezaji wa kulipwa, Boca Junior alikataa kulitoa kovu hilo. West Ham pia walijaribu kutaka kumfanyia matibabu ili kumuweka sawa lakini amebaki na kumbukumbu hiyo.

Tevez alivunjwa meno katika ugomvi na wenzake mtaani kwao Fuerte Apache utotoni.

Tevez anasema anashukuru amechagua njia sahihi kwani angeweza kuwa mharifu, muuza unga na ukabaji lakini soka limemtoa na sasa sio masikini tena anaishi kwa amani.

 



Comments