CARLOS BACCA amezipiga chini miamba                    ya Premier League - Liverpool na Manchester United na                    kuamua kujinga na AC Milan ya Italia.
              Bacca amekubali dili hilo baada ya                    AC Milan kuweka mezani pauni milioni 21.5 ambazo                    zimetosha kufikia kipengele cha manunuzi kilichowekwa                    kwenye mkataba wake.
                                                                           "Carlos amechagua kilicho bora                      kwa maisha yake, ana furaha kubwa"
                             Sergio Barila
            
                          Ripoti                  kutoka Italia zinasema Carlos amepewa ofa ya pauni                  milioni 1.8 kwa mwaka ambayo inaweza ikaongezeka hadi                  2.5 kama atang'ara San Siro.
                                       Nathibitisha                  kuwa Milan na mchezaji wamefikia makubaliano," Sergio                  Barila, mwakilishi wa Bacca aliliambia gazeti la Milan                    News la nchini Italia.
                                       "Bacca amechagua                    kilicho bora kwa maisha yake, ana furaha kubwa.                    Itachukua muda gani dili kukamilika? hilo sasa                    waulizeni AC Milan," anaeleza Sergio Barila
                                       Liverpool                  na Manchester United walikuwa wakimwania mshambuliaji                  huyo aliyeifungia Sevilla magoli 28 msimu uliopita.
                                
Comments
Post a Comment