BASTIAN SCHWEINSTEIGER ANUKIA MANCHESTER UNITED ...akataa mkataba mpya Bayern, Franz Beckenbauer anapotea njia




BASTIAN SCHWEINSTEIGER ANUKIA MANCHESTER UNITED ...akataa mkataba mpya Bayern, Franz Beckenbauer anapotea njia
BASTIAN SCHWEINSTEIGER anatajwa kuwa yuko njiani kujiunga na Manchester United.
Gazeti la kila siku la L'Equipe la Ufaransa limeripoti kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 30, amekataa mazungumzo ya mkataba mpya Bayern Munich ili kusafisha njia ya kwenda Old Trafford.
United inatarajiwa kulipa pauni milioni 17.8 ili kumnyakua mchezaji huyo mshindi wa kombe la dunia.
Bastian              Schweinsteiger man utd transfer news
ANAKARIBI: Schweinsteiger njiani kutua Manchester United
"Namshauri asiende England, abakie hapa"
Franz Beckenbauer
Hata hivyo gwiji wa Bayern Franz Beckenbauer amemtaka Schweinsteiger asikubali kwenda Manchester United.
Beckenbauer amesema: "Binafsi ningemshauri asiende England na abakie hapa. Hizi changamoto mpya anazotafuta katika umri huo, si sahihi"



Comments