BASTIAN SCHWEINSTEIGER AIKATA MAINI MANCHESTER UNITED ...asema anabaki Bayern Munich




BASTIAN SCHWEINSTEIGER AIKATA MAINI MANCHESTER UNITED ...asema anabaki Bayern Munich

BASTIAN SCHWEINSTEIGER ameitolea mbavuni Manchester United kwa kusema anafikiria kumalizia soka lake Bayern Munich.

Boss wa United Louis van Gaal alionyesha nia ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani na alikuwa tayari kulipa pauni 10.

Inaaminika United ilishaanza kufanya maongezi na nyota huyo mwenye umri wa miaka 3, lakini sasa Schweinsteiger anakuja na habari mbaya kwa wapenzi wa Manchester United.

Schweinsteiger anasema angependa kubaki Bayern na kuisaidia kuendelea kushinda mataji ikiwa ni pamoja na kuipa nguvu timu hiyo ili iwe klabu ya kwanza Ujerumani kushinda taji la Bundesliga mara mfululizo.
HAENDI KOKOTE: Bastian Schweinsteiger aichomolea Man United
Mshindi huyo wa kombe la dunia anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa kuitumikia Bayern Munch, lakini anatarajiwa kuurefusha mkataba huo kabla msimu mpya haujaanza.
"Najisikia vizuri na nipo tayari kucheza kwa miaka mitatu ijayo kwenye kiwango cha juu. Hayo ndio malengo yangu"
Bastian Schweinsteiger

Schweinsteiger amesema:"Tumeshinda taji la Bundesliga mara tatu mfululizo, hakuna timu iliyowahi kushinda mara nne mfululizo. Hiyo ndio kiu yangu. 

"Najisikia vizuri na nipo tayari kucheza kwa miaka mitatu ijayo kwenye kiwango cha juu. Hayo ndio malengo yangu."





Comments