BAADA YA KUTUA RASM ARSENAL PETR CECH ANENA: "BADO NINA NJAA YA MAFANIKO ...ASANTE WENGER"



BAADA YA KUTUA RASM ARSENAL PETR CECH ANENA: "BADO NINA NJAA YA MAFANIKO ...ASANTE WENGER"


Petr Cech amekamilisha rasmi usajili wake Arsenal baada ya kufuzu vipimo vya afya na akasema bado ana njaa ya mafanikio.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 anatua Arsenal kwa ada ya pauni milioni 10 baada ya kuitumikia Chelsea kwa miaka 11. 
"Petr Cech amethibitisha kuwa ni mmoja wa makipa bora duniani na atatuongezea nguvu kwenye kikosi chetu"
Arsene Wenger
Muda mfupi baada ya kutambulishwa rasmi Arsenal, Cech akasema anafurahi kujiunga na timu kubwa kama Arsenal na anashindwa kusubiri siku ya kuanza maandalizi ya msimu mpya akiwa na timu yake mpya.
Cech alisema: "Nina furaha sana kujiunga na Arsenal, wajibu wangu katika soka ni ule ule, ari ile ile na njaa ile ile ya mafanikio niliyokuwa nayo tangu nilipoanza maisha yangu ya soka.
"Namshukuru sana kocha Arsene Wenger kwa kuamini kuwa ninaweza kuwa kwenye mipango yake, mara ya kwanza aliponiambia kuwa ananihitaji nilifurahi na sikuwa na ubishi."
Naye Arsene Wenger alisema: "Katika misimu mingi,  Petr Cech amethibitisha  kuwa ni mmoja wa makipa bora duniani na atatuongezea nguvu kwenye kikosi chetu.
"Petr Cech ni mchezaji niliyemtamani kwa muda mrefu na nina furaha kuwa amekubali kujiunga nasi."


Comments