ATLETICO MADRID KUIPIGA CHINI OFA YA CHELSEA KUMTAKA ANTOINE GRIEZMANN



ATLETICO MADRID KUIPIGA CHINI OFA YA CHELSEA KUMTAKA ANTOINE GRIEZMANN
Chelsea imekula za uso katika mbio zao za kusaka saini ya mshambuliaji  maridadi wa Atletico Madrid Antoine Griezmann.
NGOMA NZITO: Chelsea ipo katika wakati mgumu katika mbio za kumwania Antoine Griezmann
Chelsea ilikuwa tayari kutoa pesa pamoja mchezaji mmoja kati ya Filipe Luis na Mo Salah ili kumpata nyota huyo mwenye thamani ya pauni milioni 43.
Atletico wanataka pesa kamili huku kocha wao Diego Simeone akitarajiwa kutoa maoni ya kupigwa chini kwa ofa ya Chelsea pindi atakapokutana na wakurugenzi wa klabu wiki hii.
Inaaminika klabu hiyo ya Hispania itashawishika kumuuza Griezmann iwapo ofa ya pauni milioni 43 itawekwa mezani - lakini Chelsea kwa sasa haina mpango wa kulipa pesa ndefu kiasi hicho.



Comments