ASHLEY YOUNG AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA KIPENZI CHAKE CHA UTOTONI ...ni miaka minne baada ya 'harusi' ya kwanza kuvunjika saa 48 kabla haijakamilika
Ashley Young amefurahia msimu wake mzuri na Manchester United kwa kufunga ndoa na kipenzi chake cha tangu utotoni Nicky Pik - miaka minne baada ya harusi yao ya kwanza kuvunjika masaa 48 kabla haijafungwa.
Winga huyo wa England aliwaacha hoi ndugu na mafariki zake wakati alipovunja sherehe za harusi yake yenye thamani ya pauni 200,000 siku mbili kabla ya kufungwa kwa ndoa hiyo mwaka 2011.
Lakini safari hii wapenzi hao walioanza mahusiano tangu wakiwa shule, imefanyika kwa siri salama salmin Jumamosi iliyopita katika hotel ya Stoke Place huko Buckinghamshire.
Ashley Young (kushoto) akiwa na mkewe Nicky Pike (wa pili kushoto) wakiwa na rafiki zao
Comments
Post a Comment