ARSENAL YAMTUMIA SANCHEZ KUMSAJILI VIDAL KWA PAUNI MILIONI 21


ARSENAL YAMTUMIA SANCHEZ KUMSAJILI VIDAL KWA PAUNI MILIONI 21
Arsenal inaangalia uwezekano wa kumtumia  mshambuliaji wake Alexis Sanchez kumshawishi mchezaji mwenzake wa Chile Arturo Vidal kutua Emirates.
Washika bunduki wa London wanatajwa kuwa wapo tayari kuweka mezani pauni milioni 21.3 kwa Juventus ili kumpata Vidal.
Kwa mujibu wa habari kutoka Hispania, Sanchez amekuwa akifanya juhudi za kumvuta Vidal Arsenal huku ikidawa Juventus wako tayari kumpiga bei kama pesa nene itawekwa mezani.
Kwasasa nyota hao wawili wako pamoja wakiitumikia Chile kwenye michuano ya Copa America.
EMIRATES : Arsenal inamtaka Vidal
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger  anaangalia namna ya kuboresha safu yake  ya kiungo na ulinzi ili kupigania vema mataji msimu ujao. 
Vidal, 28 amekuwa na kiwango cha hali ya juu kwa muda mrefu tangu alipokuwa akiicheza Bayer Leverkusen ya Ujerumani kabla hajahamia Juventus mwaka 2011. 



Comments