Tetesi mpya za usajili ligi kuu ya              England zinasema Arsena imefikia makubaliano ya kumsajili              kiungo wa Chile na Juventus Arturo Vidal mwenye umri wa miaka 28.
          Kwa mujibu wa gazeti la  La Stampa, la Chile,              Vidal ameuzwa Arsenal kwa pauni milioni 21.
        Gazeti hilo limeeleza kuwa usajili              wa kiungo huyo mwenye nguvu, bingwa wa kuharibu mipango ya              timu pinzani na mmaliziaji mzuri anapokuwa jirani na goli la              adui, atatangazwa rasmi muda mfupi baada ya michuano ya Copa              America kumalizika wiki ijayo.
          Juventus tayari                wameshamsajili Sami                Khedira kama mbadala wa Vidal na pia wahahitaji kuuza                mchezaji kabla hawajasili chaguo lao lingine.
          Mabingwa                hao wa Italia wanataka kumsajili Mehdi Benatia kutoka                Bayern Munich ili kuimarisha zaidi safu yao ya ulinzi.
          Vidal ni kiungo anayesakwa zaidi              na vilabu vingi barani Ulaya baada ya kuwa na misimu mitatu              ya mafanikio Turin.
          Msimu                uliopita, Vidal alikuwa chaguo kuu la kocha wa Manchester                United, Van Gaal lakini Juventus wakakataa kumuuza.
          
Comments
Post a Comment