ARSENAL YAMKANA VIDAL ...hayuko kwenye rada za Arsene Wenger



ARSENAL YAMKANA VIDAL ...hayuko kwenye rada za Arsene Wenger Arsenal imesema haina mpango wa kumsajili kiungo wa Juventus, Arturo Vidal, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza.


Habari hiyo zinakuja baada ya gazeti moja la Italia La Stampa kuandika jana kuwa Washika bunduki wa London wamefanikiwa kumsajili Vidal kwa pauni milioni 21.
Arsenal waliripotiwa kuwa wamekuwa wakimfukuzia Vidal kwa miezi kadhaa.
Lakini habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimenukuliwa na The Sun ziksema Vidal hayuko kwenye rada za kocha wa Arsenal Arsene Wenger.

Arsenal Transfer News Arturo Vidal
HAKUNA MPANGO: Arsenal imemkana Vidal


Comments