Colombia imetolewa na Argentina kwa njia ya 'matuta' kwenye robo fainali ya Copa America, lakini kama kuna mtu aliyelazimisha mechi hiyo iende hatau ya mikwaju ya penalti basi ni kipa wa Colombia David Ospina.
Ospina ambaye pia ni mlinda mlango wa Arsenal aliwanyima Argentina magoli mengi ya wazi kwa kupangua michomo mingi kwa namna ya ajabu.
Kipa huyo ambaye yuko njiani kuondoka Arsenal kufuatia ujio wa Petr Cech, aliokoa kwa mguu mkwaju wa Auguero ambao dhahiri ulikuwa unakwenda kutinga wavuni.
Ospina akawaduwaza watu pale alipopangua mpira wa kichwa wa Lionel Messi, kabla kumnyima goli Nicolas Otamendi.
Argentina walitawala mpira kwa muda wote wa mchezo lakini kipa David Ospina alikuwa kikwazo kwao.
Kwa muda wote wa michuano ya Copa America, Ospina amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, hali inayotoa picha mbili – ya kwanza ni kwamba bei yake lazima ipande na ya pili Arsenal lazima watajuta kumuuza.
Ni wazi kuwa kipa huyu mwenye umri wa miaka 26 atakuwa mmoja wa makiba bora duniani.
David Ospina akizuia mpira wa kichwa wa Lionel Messi
Aguero haamini kuwa mpira wa Messi umechezwa na Ospina
Messi na Aguero ni kama hawaani kinachotokea kwa Ospina huku Angel di Maria akienda kupiga mpira wa kona
Messi akiduwaa kwa ubora wa Ospina
Nicolas Otamendi akilaani baada ya Ospina kumnyima bao
Ospina anaruka mbizi kuzuia Javier Pastore asilete madhara
Kipa wa Arsenal alifanya kosa la kumiliki mpira lakini akawa mwepesi kumzuia Aguero asifunge
Comments
Post a Comment